UEFA Yafanya Mabadiliko Katika Michuano Ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League


Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limefanya baadhi ya mabadiliko katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya na Europa League, mabadiliko hayo yataanza msimu ujao 2018/19.

Timu zitaruhusiwa kufanya mabadiliko (Sub) ya nne endapo mechi itaenda "Extra Time" katika hatua ya mtoano.

Mara zote katika mechi za michuano hiyo, ni wachezaji 18 huandikwa katika karatasi ya mechi, 11 wanaanza huku 7 wakiwa benchi, kuanzia msimu ujao itakuwa ni hivyo hivyo katika mechi zote kasoro mechi za Fainali Klabu Bingwa Ulaya, Fainali Europa League na UEFA Super Cup, ambapo katika mechi hizo karatasi la mechi litajumuisha wachezaji 23, 11 wanaanza huku 12 wakiwa benchi. Hii itawapa makocha uwanja mpana wa kuchagua wachezaji katika mechi hizo muhimu.

Mabadiliko mengine ni katika usajili, timu zitaruhusiwa kusajili wachezaji wapya watatu baada ya mechi za makundi bila ya vizuizi vyovyote, hivyo makocha watapata uhuru zaidi katika sajili zao katika dirisha la januari.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.