Dr Congo Waiona Shule Waliyoipata Stars Kutoka Algeria..


Na Alexander Victor.
Licha ya kusheheni wachezaji kadhaa wanaosakata kandanda ndani na nje ya bara la Afrika, timu ya taifa ya Congo Dr '' Leopard" imekubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Tanzania "Taifa stars".

Magoli ya Stars yamefungwa na nahodha wa timu hiyo na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta mnamo dakika ya 74' baada ya kupokea krosi mujarabu iliyopigwa na Shiza Kichuya na kuunganisha mpira ule kwa kicha na kujaa kambani.

Huku goli la pili limepatikana mnamo dakika 86' kupita kwa yule aliyetengeneza goli la kwanza nikimaanisha Shiza Kichuya baada ya kumalizia kwa ugundi mkubwa mpira uliopigwa na nahodha Mbwana Samatta na kuiandikia Stars goli la pili na la Ushindi katika Mchezo huo.

Baada ya mchezo makocha wote wamezubgumza na waandishi wa habari huki kocha msaidizi bora wa Tanzania Hemed Morocco amesema walijiandaa vyema na wametumia udhaifu wa apinzani wao kuwa wazito kupata matokeo.

Aidha kocha wa Leopard amesema safu nzuri ya ushambuliaji imefanya ilichotakiwa kifanya huku akipeleka lawama kwa wacheza wake kwa kushindwa kumiliki mipira na kuigawa kwa wapinzani...

Mchezo huo ulikuwa wa pili kwa Stars baada ya ule wa awali iliocheza dhidi ya Algeria na Stars kupoteza kwa goli 4-1 hivyo leo walikuwa wakijaribu kutumia mbinu za kulinda heshima ya uwanja wa nyumbani na kuhakikisha wanaondoa makosa waliyoyafanya kwa Algeria.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.