Tetesi za Usajili Ulaya Leo Jumanne 27.03.2018






Meneja wa Manchester United Mourinho ameandaa orodha ya wachezaji sita ambao anaamini wanaweza kujaza nafasi ya Michael Carrick anayeelekea kustaafu. Orodha hiyo inashirikisha nyota wa Bayern Munich kutoka Chile Arturo Vidal, 30, na Mwitaliano anayechezea Paris St-Germain Marco Verratti, 25. (Manchester Evening News)


Barcelona wanapanga kuwasilisha ombi la kutaka kumchukua beki wa Manchester United Luke Shaw mwisho wa msimu. Beki huyo wa kushoro wa miaka 22 kutoka England amekosolewa sana na meneja wa United Jose Mourinho wiki za karibuni. (Mirror)

Mabingwa wa Ufaransa Monaco ndiyo klabu ya karibuni zaidi kuonesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ubelgiji unamalizika mwisho wa msimu na anatarajiwa kuondoka Old Trafford. (Mail)

Dani Ceballos ambaye amekuwa akitafutwa na Liverpool ameambia anaweza kutoka Real Madrid mwisho wa msimu. Kiungo huyo wa kati Mhispania wa miaka 21 amekuwa pia anatafutwa na AC Milan na Juventus. (Mundo Deportivo kupitia Talksport)

Kipa Mbelgiji Simon Mignolet, 30, amesema atasalia na kupigania nafasi yake katika kikosi cha kwanza Liverpool na hatalazimishwa kuondoka klabu hiyo. (Sun)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema anataka sana kiungo wa kati Jack Wilshere asalie katika klabu hiyoo. Mchezaji huyo wa England wa miaka 26 amekuwa kwenye mvutano na klabu hiyo kuhusu mkataba baada yake kuombwa akubali kupunguziwa mshahara. (Star)

Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel angependa zaidi kwenda Bayern Munich kurejelea kazi ya ukufunzi na si kwenda Arsenal, kama zilivyokuwa zimedokeza tetesi kwamba atakwenda kumrithi Wenger. (Sky Sports) Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Thomas Tuchel

Kiungo wa kati wa Liverpool kutoka Ujerumani Emre Can, 24, amelazimika kuandika kwenye Instagram ujumbe wa kupuuzilia mbali uvumi kwamba anataka kuondoka Anfield.

United wataimarisha juhudi zao za kutaka kumnunua beki wa Celtic ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £25m Kieran Tierney mwisho wa msimu. Mourinho anataka sana beki huyo wa miaka 20 mzaliwa wa Manx, Scotland ajiunge na klabu hiyo na anatarajiwa kuwasilisha ofa karibuni. (Mirror)

Mchezaji nyota wa Brazil Ronaldinho amefichua wkamba alikuwa saa 48 karibu na kujiunga na United mwaka 2003 kujaza nafasi ya David Beckham aliyekuwa amehamia Real Madrid. Badala yake mchezaji huyo wa miaka 38 alijiunga na Barcelona pale Sandro Rosell alipoteuliwa rais wa klabu hiyo. (FourFourTwo)

Kiungo wa kati Mbelgiji anayechezea Chelsea Eden Hazard amepuuzilia mbali wanaomfananisha na nyota wa Barcelona Lionel Messi. Mchezaji huyo wa miaka 27 amesema yeye huwa hafungi mabao mengi kiasi cha kufananishwa na nyota huyo wa Argentina. (Star)

Hazard amesema kwa sasa atapatia kipaumbele kuchezea timu yake ya taifa Kombe la Dunia badala ya mazungumzo kuhusu mkataba mpya Chelsea. (Guardian)

Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois amesema bado atakuwa Stamford Bridge msimu ujao hata kama hakutakuwa na maafikiano kuhusu mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa mlindalango huyo wa miaka 25 kutoka Ubelgiji unamalizika Juni 2019. (Sporza kupitia Telegraph) Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Thibaut Courtois

Chama cha Soka England FA kinapanga kuwa kikichunguza mechi zote ambazo timu taifa hilo itakuwa incheza Ijumaa usiku baada ya mashabiki wa taifa hilo kuzua fujo Amsterdam wiki iliyopita. (Times)

Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucoure amesema ni ndoto yake kuchezea klabu ya Liverpool. Mfaransa huyo wa miaka 25 amehusishwa na kuhama klabu hiyo ya Vicarage Road. (Express)

Kiungo wa kati wa Leicester City Andy King ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu. Mwingereza huyo wa miaka 29 alijiunga na Swansea kwa mkopo Januari na anapangiwa kuhamia klabu hiyo ya Wales kwa mkataba wa kudumu Wales. (Leicester Mercury)

Brighton na Bournemouth wanapanga kujaribu kumnunua winga wa Celtic Scott Sinclair, 29, na kumrejesha Ligi ya Premia. Sinclair alijiunga na Celtic kutoka Aston Villa mwaka 2016. (Mail) Haki miliki ya picha SNS Image caption Scott Sinclair

Pierre-Michel Lasogga ambaye yupo Leeds United kwa mkopo amesema hataki kurejea klabu yake ya Hamburg huku akiendelea kukimbiza ndoto yake ya wakati mmoja kuchezea Ligi ya Premia. Mshambuliaji huyo kutoka Ujerumani ambaye ana miaka 26 amefunga mabao 10 tangu ajiunge na Leeds mwaka jana. (Bild)



Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.