Taarifa iliyotufikia Asubuhi Hii Kutoka Yanga
Kikosi cha Yanga kimerejea Alfajiri ya leo kutoka nchini Botswana kushiriki mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers.
Licha ya suluhu ya bila kufungana iliyopata kwenye mchezo huo, Yanga iliondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kufuatia kipigo cha mabao 2-1 nyumbani.
Hata hivyo Yanga bado ina nafasi moja ya kujaribu kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho ambapo droo ya michuano inatarajiwa kufanyika keshokutwa Jumatano Cairo, Misri.
Waachezaji Ramadhani Kabwili, Hassani Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Ibrahim Ajib wamejiunga na kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kitakachocheza mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Algeria, March 22.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.