Simba Yaipiku Yanga Kwa Hili.


Mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Simba ya jijini Dar es Salaam na Al Masry ya Misri umeingiza pesa nyingi zaidi ya ule wa klabu Bingwa Afrika kati ya Dar Young Africans na Township Rollers ya Botswana.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini (TFF) umeonesha kuwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Yanga na Township Rollers uliochezwa Jumanne Machi 6, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi Milioni Hamsini na Sita laki mbili na elfu arobaini na tano(56,245,000).

Mchezo huo uliingiza mashabiki Elfu Tisa Mia Tisa Sitini na Moja (9,961).

“VIP A waliingia Watazamaji Tisini na Tisa(99) kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 1,980,000, VIP B na C waliingia Watazamaji 991 kwa kiingilio cha shilingi 10,000 ikapatikana jumla ya shilingi 9,910,000,majukwa ya rangi ya Machungwa,Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 8,871 kwa kiingilio ncha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 44,355,000,” imesema taarifa hiyo.

Mechi ya Simba

Aidha katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliozikutanisha Simba na Al Masry uliochezwa Jumatano Machi 7, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi Milioni Themanini na Tano Elfu Arobaini na Tano (85,045,000).

“VIP A waliingia Watazamaji 250 kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 5,000,000,VIP B na C waliingia Watazamaji 557 kwa kiingilio cha shilingi 15,000 ikapatikana jumla ya shilingi 8,355,000,majukwa ya rangi ya Machungwa,Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 13,644 kwa kiingilio ncha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 68,220,000,” imeongeza taarifa hiyo.

Mchezo huo uliingiza mashabiki Elfu Kumi na Nne Mia Saba Tisini na Nane (14,798).
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.