Simba Yaanza Kujiandaa Kuwakabili Waarabu
Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba kimerejea mazoezini leo kujiandaa mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa wiki ijayo, March 17 nchini Misri.
Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre ameongoza mazoezi hayo yanayofanyikwa katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es salaam.
Baada ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa juzi, Simba itakwenda Misri kuhakikisha inapata ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao 3-3.
Sare ya mabao 2-2 itapelekea mshindi kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati kama hatapatikana mshindi katika muda wa nyongeza.
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.