Niyonzima Akamilisha Matibabu Sasa Kurejea Nchini. Fahamu Siku Ya Kurejea Kwake Hapa>.>>>
Kiungo Haruna Niyonzima amekamilisha matibabu yake nchini India na sasa anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki, imefahamika.
Niyonzima alikwenda India kutibiwa majeraha ya goti wiki iliyopita.
"Nimepata matibabu mazuri na ambayo yananipa moyo kuwa nitarejea uwanjani mapema, ninaumia kutoisaidia klabu yangu katika mbio za ubingwa, ila yote hii ni mipango ya Allah," alisema nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi).
"Kuhusu nitarudi lini uwanjani, nitajua kesho baada ya kukutana na daktari wangu, ila kifupi nitarejea mapema sana tofauti na nilivyokuwa natarajia kabla ya kuja India, na safari yangu itakuwa karibuni"
Niyonzima hajaitumikia Simba tangu mwishoni mwa mwaka 2017 akisumbuliwa na majeruhi ya aina tofauti tofauti.
Wakati anakwenda India, Msemaji wa Simba Haji Manara alisema anatarajiwa kuwa nje kwa wiki mbili kabla ya kurejea dimbani baada ya kukamilisha matibabu yake.

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.