'Mpapasaji Kapapaswa' (Masau Bwire).
Raundi ya 20 ya ligi kuu Tanzania bara imeendelea kwa michezo kadhaa kupigwa hapo jana amvapo mmoja kati ya michezo hiyo ni ule uliozikutanisha klabu za Njombe mji na Ruvu Shooting.
Katika mchezo huo wenyeji Njombe mji waliibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting kitu ambacho wadau wengi wa soka wamesema kuwa ni hali ya mtenda kutendewa.
Kauli hii imekuja baada ya kauli aliyoitowa msemaji wa Ruvu Shooting muda mchache kabla ya Pambano hilo kuanza akidai kuwa kilichowapeleka Njombe ni kuipapasa Njombe mji FC
Aidha baadhi ya mashabiki wameongeza na kusema kuwa "Mpapasaji Kapapaswa"..
FT Njombe Mji 2-1 Ruvu Shooting
27' Nchimbi 32' Mtuwi
56' Mwasondola
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.