Manara Awashukia Mashabiki Wa Yanga..


Afisa habari wa klabu ya Simba sc, Haji Manara amewamewashakaa mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa wakichambua sababu za vilabu kupoteza mechi za nyumbani na kudai kuwa ni kukosa uzalendo..

Manara kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika:
"Naona huko mitandaoni baadhi ya wanayanga wanataja sababu mojawapo ya timu za bongo kutofanya vzuri uwanja wa nyumbani ni kukosa uzalendo kwa vilabu vyetu....wanalosahau wao nililisema hadharani mapema na nikabezwa na viongozi wao..leo ndio mwaujua uzalendo?Nawaambia kwa sasa tutafanya zaid yenu..kama tudini tudani....uzalendo wetu utabaki kwa timu za Taifa tu"

Kauli za Haji Manara kufuatia Simba kutolewa na Al Masry jana

"Why sijaangusha chozi jana usiku? Wachezaji walipigana kwa nguvu zao zote. Niliiona fighting spirit ya jasho na damu. Niliiona hassle ya wanaume dimbani, nilimuona Juuko nayemjua, nilimuona Aishi Tz one, nilimuona Mkude halisi,nilimuona Erasto aliyekunja uso dk 90"

" Ntaamini mpira haraam kama wanaume wale wa Jana watashindwa kuifunga Yanga na kuchukua ubingwa wa VPL. Nitawaambia kweupe wachezaji,kwa ubora mlio nao mkishindwa kutupa ubingwa nitawaandika kwa kalamu ya wino wa damu kwenye moyo wangu..."

 " Sio tu kwamba ntawachukia wachezaji ila ntauchukia mchezo wa Soka na ntakaa pembeni kujihusisha na mchezo huu ulionisaidia kunikuza,kunilea na kunisomesha. Mimi ni mtu wa misimamo na ntalisimamia hilo kwa kiapo cha watoto wangu. "

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.