Licha Ya Mvua Kubwa Kunyesha Mechi Imemalizika Tu. Haya Hapa Matokeo Ya Simba vs Al-masry..


Licha Ya Mvua kubwa iliyonyesha katika jiji la Dar es Salaam lakini mpira kati ya Simba na Al-Masry umemalizika kwa timu hizo  kutoshana nguvu kwa sare ya goli 2-2 .

Simba ndio walioanza kulitazama goli la wapinzani mnamo dakika ya 9' kupitia kwa John Bocco na Al-Masry kuswazisha kupitia mnamo dakika ya 11' yaani dakika 2 baadae kupitia kwa Ahmed Gomaa.

Mnamo dakika ya 25 Al-masry waliongeza bao mnamo dakika 25 kupitia kwa Ahmed Abdalraof na Simba kusawazisha kwa Emmanuel Okwi  dakika 74'.

Wakati presha ikiendelea kuwazidia Al-masry mvua inashuka na kuufanya mpira usimame na baada ya mvua kupungua mpira kuendelea.

Wakati wakirejea umahili wa mchezo ukapungua na kushuhudiwa mipira ikibutuliwa kutokana na halo ya uwanja kutapakaa maji katika sehemu kubwa..

Na kwa matokeo hayo basi Simba italazimika kuhakikisha inapata ushindi ugenini au kama ni sare basi kuanzia magoli 3-3 na kuendelea ili kuhakikisha inasonga katika nafasi inayofuata.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.