Kocha Wa Congo Awataja Wawili Walioisumbua Timu Yake Hadi Kufungwa, Hawa Hapa..
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imewato kimasomaso Watanzania baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Mabao yote ya Stars yalipatikana katika kipindi cha pili wafungaji wakiwa Mbwana Samatta na Shiza Kichuya.
Baada ya kumalika kwa mchezo huo kocha mkuu wa Congo, Florent Ibenge amewamwagia sifa Nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Simon Msuva kutokana na aina ya uchezaji waliouonyesha katika pambano hilo.
Akizungumzia namna timu yake ilivyo cheza amesema timu yake haikuwa makini sana kwani walipoteza mipira kwa wapinzani.
"Wana safu.nzuri ya ushambuliaji yenye watu kama Samatta na Msuva ambao wameonyesha mpira mzuri, tulipoteza mipira mingi na tuliwapatia mipira mingi na ndio maana wakapata nafasi na wakazitumia." Alisema Ibenge.
Mchezo huo ulio kwenye kalenda ya FIFA uliishuhudia Stars ikicheza kandanda safi ya kujilinda na kushambulia tofauti na mchezo uliopita.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.