KOCHA LWANDAMINA AZUNGUMZIA KADI ZA CHIRWA TSHISHIMBI.
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina amezungumzia juu ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao watakosekana katika mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) dhidi Wolaitta Dicha ya Ethiopia.
Yanga ambayo ilitua kunako shirikisho baada ya kuondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika(CAF Champions League) watawaalika Wolaitta Dicha ambayo ilifika hatua hiyo kwa kuwaondoa klabu ya Zamalek kutoka Misiri.
Katika mchezo huo wacheaji kadhaa watakosekana kutokana na kuadhibiwa kwa kadi za njano katika michezo ya klabu bingwa ambapo kwa mujibu wa sheria za CAF mchezaji anapokuwa na kadi mbili za njano basi analazimika kuukosa mchezo unaofuata, Wachezaji ambao wataukosa mchezo huo ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi na Said Jumma Makapu
Lwandamina amesema hana jinsi ya kufanya kutoka na kuwakosa wachezaji hao katika mechi yao ya kombe la shirikisho barani na badala yake atawatumia wachezaji wengine.
"Nitatumia wachezaji niliokua nao ili kuweza kujiandaa kwa ajili ya mchezo huotutafanya maandalizi ya pamoja ya kombe la FA dhidi ya Singida United na kombe la Shirikisho Afrika ambayo siwezi kuyatenganisha kwa sababu mechi zinakwenda sambamba". Alisema Lwandamina.
Ikumbukwe kuwa Yanga itawaalika Waethiopia hao mapema mwezi ujao katika mchezo wa awali wa Play off ya Kombe La Shirikisho na kurudiana siku kadhaa Nchini Ethiopia.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.