Hii Ndio Siku Ambayo Simba Na Al - Masry Zitamenya Na Hivi Hapa Viingilio Vya Mchezo huo.


Klabu ya Simba itacheza mchezo mwingine katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al-Masry uliopangwa kuchezwa Jumatano ijayo tarehe 7.3.2018 katika uwanja wa Taifa. 
Katika kuwajali na kuthamini mchango wa mashabiki na wapenzi wa Simba pamoja na mchezo wa soka, sasa mchezo huo utapigwa saa 12:00 jioni badala ya 10:00 jioni ili kuweza kuwapa fursa mashabiki wengi zaidi kupata nafasi ya kuja uwanjani na kuipa sapoti timu yao. 
Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Haji Manara alifafanua hili 'Tumepeleka mbele muda na kuwa saa 12:00 jioni ili kuwapa nafasi mashabiki wetu wengi zaidi kuja uwanjani na kuipa sapoti timu yao kwani sote tunafahamu kuwa Jumatano ni siku ya kazi na wengine wetu watakuwa makazini' 

Kikosi cha Al-Masry kinatarajiwa kutua nchini Kesho ambapo kitafanya mazoezi jioni Jumatatu katika uwanja wa Taifa. 
Kuhusiana na viingilio katika mchezo huo Haji amevitaja viingilio kuwa 
Orange na Mzunguko - Tsh 5,000/=
VIP B - 15,000/=
VIP A - 20,000/=

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.