Hii Hapa Taarifa Mpya Kutoka Simba Juu Ya Maendeleo Ya Jonas Mkude.
BAADA ya juzi kuumia akiwa kwenye mazoezi na kuleta hofu, kiungo wa Simba, Jonas Mkude, anatarajiwa kurejea uwanjani kesho kuendelea kujifua ili kuisaidia timu yake kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Mkude aliumia na kubebwa juu juu wakati akiwa kwenye mazoezi juzi, jambo ambalo liliwafanya mashabiki wa timu yake kuingiwa na hofu ya kumkosa nyota huyo kwa muda mrefu.
Akizungumza na gazeti la Nipashe, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara, alisema kuwa kiungo huyo alipata majeraha madogo na baada ya vipimo alivyofanya jana, atarejea uwanjani mapema.
Manara alisema taarifa ya daktari inaonyesha kuwa Mkude atakuwa ameshapona kabla ya safari ya kuelekea Njombe kuwafuata wenyeji wao Njombe Mji FC na kuwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo wasiwe na wasiwasi kuhusu kiungo huyo.
"Mkude alipata mchubuko katika ngozi karibu na mfupa wa enka, daktari amesema ni maumivu madogo na atarejea kwenye mazoezi kati ya kesho (leo) au keshokutwa (kesho)," alisema kwa kifupi afisa huyo.
Aliongeza kuwa wachezaji wengine wanaendelea vyema na mazoezi na wamejipanga kupambana ili kusaka ushindi kwa mechi zote zilizobakia za ligi hiyo inayotarajiwa kumalizika ifikapo Mei 26, mwaka huu.
"Tunajua tuko kwenye vita ya ubingwa, hatutaki kumsemea mtu mwingine, tumeiona ratiba mpya na tutacheza mechi kama zilivyopangwa kwa sababu imezingatia kanuni ya tofauti ya saa 72 baina ya mechi moja na nyingine," aliongeza Manara.
Simba inatarajia kuondoka jijini kuwafuata wenyeji wao Njombe Mji katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe na baadaye kuelekea Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar Aprili 9 mwaka huu.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.