Hii Hapa Taarifa Kutoka Misiri Iliko Timu Ya Simba Usiku Huu..


Kwa mujibunwa taarifa zilizotufikia usiku huu kutoka Misiri ambako Simba imekwenda kushiriki mchezo wa  marudiano kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al-masry Zinaeleza kuwa klabu ya Simba imepata makaribisho mazuri tofauti na ilivyotarajiwa na wengi.

 Mara baada ya mapokezi timu hiyo imepewa uwanja wa mazoezi ambayo imeanza kuyafanya usiku wa jana. Na kuendelea usiku huu.

Licha ya baridi kali iliyopo katika eneo hilo lakini inaelezwa kuwa wacheza wote wapo katika hali nzuri wala hakuna mgonjwa wala majeruhi miongoni mwa wachezaji walioko huko.

Msafara wa klabu hiyo unaongozwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), James Muhagama na Kaimu Raisi wa Simba ,Salimu Abdallah , wajumbe wa kamati ya utendaji na wajumbe wa sekretarieti pamoja na wanachama.

Aidha imeelezwa kuwa wachezaji wote wanamorali a kutosha na hii imechangiwa na mapokezi mazuri na hivyo kuwafanaya baadhi ya wanachama kuwa na matumaini ya kupata matokeo mazuri.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.