HABARI KUBWA KATIKA SOKA TANZANIA LEO ALHAMISI MARCH 1.2018


Yanga yafuta uteja huko Mtwara hapo jana hii ni baada ya kuifunga Ndanda sc goli 2-1 hapo jana matokeo hayo yameifanya Yanga ifikishe point zake 40 ikiwa katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
👉Mkwasa awashukuru wanaMtwara kwa kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao ya Yanga asema wao kama Yanga wanashukuru kwa sapoti kubwa walio ipata.
Yanga sc sasa inajiandaa na Mchezo wa Klabu bingwa barani afrika itarejea leo ikitokea mtwara kwa njia ya basi .
👉Baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Yanga uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa umeyapokea matokeo hayo kwa Masikitiko makubwa huku ukisema kuwa wanajipanga kwa ajili ya michezo ijayo .
👉Mrisho Ngasa hapo jana alitangazwa kuwa mchezaji bora katika mchezo kati ya Ndanda sc Vs Yanga sc Ngassa jana alicheza katika kiwango bora cha hali ya juu kwani alikua mwiba mchunga kwa Yanga .
👉Singida united tumekuja Dar kuchukua point tatu kwa wanalamba lamba afisa habari wa klabu hiyo amesema kuwa kila kitu kipo sawa kuelekea mchezo huo utakao pigwa Jumamosi katika Uwanja wa Azam complex .
👉Kuelekea Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Njombe mji dhidi ya Ruvu shooting afisa habari wa klabu ya Ruvu shooting Masau bwire amesema sasa ni zamu ya Njombe mji kupapaswa .
👉Jkt Tanzania kupitia kwa Afisa habari wa klabu hiyo amesema kuwa wao kama Jkt Tanzania wamejipanga kucheza na Timu yoyote watakayo letewa katika Hatua ya Robo fainali katika kombe la Asfc .
👉Baruani Muhuza asema kuwa Drow ya kombe la shirikisho la Azam Sports itafanyika ijumaa hii na itakua live kupitia kituo cha Runinga cha Azam tv Kupitia chanel yake ya Azam Sports 2.
👉Baada ya kupanda ligi kuu Tanzania bara Timu ya biashara ya mkoani mara imesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kupata mdhaminu wa kuidhamini timu hiyo ili ifanye vyema katika ligi kuu msimu ujao .
👉Klabu ya Lipuli jana asubuhi imeendelea na Mazoezi yake katika uwanja wa samora mjini Iringa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa na Ndanda sc jumapili hii katika dimba la Somora mjini Iringa .
👉Mnyama Simba ameendelea mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya stend united kesho ijumaa huku uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa hali ya okwi ni shwari kesho anaweza anza dhidi ya stend .

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.