Kapombe: Rekodi Sio Kigezo Tosha Cha Kuwafunga Stand United.


BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amesema licha ya kuwa na rekodi ya kuwafunga Stand United 'Chama la Wana', lakini hawana budi kujifua vilivyo kwa madai kuwa soka halikaririwi.


"Hatuwezi kucheza kwa mazoea kwani, soka halikaririwi na kila mchezaji anatafuta nafasi ya kuonekana, hivyo tunajipanga kikamilifu bila kuangalia wapinzani wetu wapo nafasi gani.”


"Tunatakiwa kushinda hiyo mechi, kwani itatufanya akili zetu ziwe vizuri dhidi ya Waarabu, ndio maana hatuwezi kupuza hata kidogo kufanya maandalizi ya mchezo huo,"anasema.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.