AMKA NA TAARIFA NJEMA HII KUTOKA YANGA


Jioni ya leo klabu ya Yanga inatarajiwa kutelemka dimbani kumenyana na Mabingwa Wa Botswana mwaka 2016/2017, Township Rollers katika mchezo wa marudiano wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Katika kuelekea katika mchezo huo kikosi kipo imara na tayari kuhakikisha wanapindua matokeo mara baada ya kupoteza mchezo wa Nyumbani kwa goli 2-1.

Ili kuthibitisha uimara huo nahodha wa Yanga, Thaban Kamusoko amesema kuwa wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

"Township Rollers ni timu nzuri tunaiheshimu na tumeona mpira wake kikubwa naamini tumejipanga kuibuka na ushindi kwa kuwa mwalimu amefanyia kazi makosa yote ya mchezo uliopita," amesema Kamusoko

Kuhusiana na maendeleo ya klabu hiyo klabu hiyo iko vizuri na mpaka kumalizika kwa mzoezi ya mwisho hakukua na majeruhi yoyote, hayo yamewekwa bayana na Mjumbe wa kamati ya utendaji na Katibu wa Kamati ya Mashindano Yanga Samuel Lukumay.

“Maandalizi yanaendelea vizuri hatukupata shida yoyote tangu tunakuja hadi tumefika, tulitembelewa na balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini ambaye ndio anasimamia pia Botswana akapata muda wa kuzungumza na vijana na kuwatia hamasa na kuwaambia katika mpira kila kitu kinawezekana kwa hiyo tunaweza kugeuza matokeo.”

“Hakuna majeruhi yoyote kiujumla kambi inaendelea vizuri bila tatizo lolote”

Mchezo wa awali uliozikutanisha Yanga na Township Rollers kwenye uwanja wa Taifa, yanga ilipoteza kwa kufungwa 2-1 hivyo inahitaji kushinda kuanzia 2-0 ili kukata tiketi ya moja kwa moja kufuzu hatua ya makundi ya vilabu bingwa Afrika.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.