Amka Na Hii Kutoka Simba, Bocco Roho Za Wanamsimbazi Mikononi Mwake.


Mabingwa wa kombe la Shirikisho Tanzania(ASFC) Simba sc wao leo wapo dimba kumenyana na Klabu ya Al-masry ya nchini Misiri katika mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kuelekea mchezo huo hali ya kikosi iko vizuri na kikosi kinamorali ya kutosha licha ya kuripotiwa kuwa na baridi . Aidha kocha mkuu wa klabu hiyo, Lechantre anaamini Bocco atakuwa kwenye kiwango bora baada ya kuumia mguu kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Bocco aliumia mguu ikiwa ni dakika ya 58 ya kipindi cha pili, na kupelekea kuondolewa huku nafasi yake ikichukuliwa na Mburundi, Laudit Mavugo.

Lechantre amesema ana matumaini makubwa kwa nahodha John Bocco kuibeba Simba inayohitaji ushindi wa baop 1-0 ili iweze kusonga mbele

Mechi ya awali iliyochezwa Tanzania, ilimalizika kwa timu zote mbili kwenda sare ya mabao 2-2.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.