Amka Na Taarifa 3 Kutoka Simba Leo Jumamosi Asubuhi (March 24.2018)


~ Kikosi cha Simba kinatarajia kuanza tena mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji FC leo Jumamosi.

Simba watakuwa wanarejea kutoka mapumziko ya muda mfupi baada ya kutoka kushiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika

~ Hata hivyo Uongozi wa benchi la ufundi la Simba umeweka sheria kali ambapo kila mchezaji akichelewa kwenye matukio maalum anakatwa shilingi laki moja.


Uongozi huo chini ya kocha Pierre Lechantre umeweka sheria hiyo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa timu hiyo inakuwa na nidhamu ya hali ya juu.


Sheria hiyo ya Simba inasema kuwa kama mchezaji akichelewa kula, akichelewa mazoezini, akichelewa kwenye basi na sehemu nyingine muhimu anakatwa kiwango hicho cha fedha.

 ~Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Njombe Mji na Simba SC uliokuwa umeahirishwa, sasa umepangwa kufanyika tarehe 3, Aprili mwaka huu, katika dimba la Sabasaba mjini Njombe.

Awali kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa Machi 11 mwaka huu, lakini uliahirishwa ili kuipa Simba nafasi ya kufanya maandalizi ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya Al Masry katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Taarifa kutoka ndani ya Bodi ya Ligi zimethibitisha tarehe hiyo, na kueleza kuwa tayari timu zote mbili zimekwishapata taarifa kwaajili ya maandalizi.

Aidha 8 April 2018 kikosi cha Simba kitashuka tena uwanjani dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.