Al- Masry Yaiponza Simba Leo.

Moja ya hofu aliyokuwa nayo kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre kabla ya mchezo dhidi ya Stand United leo ilikuwa wachezaji kufikiri zaidi mchezo ujao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry unaopigwa Jumatano ijayo, March 07.

Lechantre alitumia muda mwingi akiwa na wachezaji wake kuwapa hamasa kabla ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Kwa mara ya kwanza Simba iliyokuwa na ukuta mgumu kuliko timu zote zinazoshiriki VPL imeruhusu mabao matatu kwenye mchezo mmoja.

Mabao yote yalisababishwa na uzembe katika kukaba. Kitendo cha kuwaruhusu Stand United kurudisha mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza kiliwafanya wazidi kujiamini

Ni dhahiri yale aliyoyasema Lechantre ndiyo yaliyokuwa kichwani kwa wachezaji wa Simba kwani ni kama baadhi yao hawakuwepo uwanjani.

Aina ya makosa yaliyopelekea mabao hayo sio makosa ambayo hufanywa na wachezaji wa Simba wakiwa katika ubora wao.

Kabla ya mchezo wa leo Lechantre aliseme;

“Wachezaji wanafikiria sana kuhusu mechi ya Al Masry hivyo inamaana hawafikirii ligi kuu na hawafikiri kuwa tuna mchezo wa ligi kuu siku ya Ijumaa na ninaogopa kwani wakati mwingine kama hatujajiandaa kupambana siku ya Ijumaa tutakuwa na matokeo mabaya ndiyo maana nimekuwa karibu na wachezaji kwa sababu nataka hamasa kubwa kwenye mchezo wa Ijumaa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.