Simba Yavutwa Shati Na Mwadui...
Ligi kuu Tanzania bara imeendelea jioni ya leo huku ikishuhudiwa vinara wa ligi hiuo Simba sc ikishikwa shati na wachimba madini wa Mwadui FC.
Simba sc ndio waliotangulia kuliona lango la Mwadui kupitia kwa mshambuliaji wake John Bocco alieoachika goli safi kwa kichwa goli lililodumu mpaka kutamatika kwa kipindi cha kwanza.
Mwadui wamerejea katika dimba kumalizia dakika 45 za lala kwa buriani wakiwa wamejipanga vyema na kufanikiwa kusawazisha goli mnamo dakika ya 59 kupitia kwa DaviD Luhende kwa mpira wa adhabu uliopigwa na kugonga mtambaa wa panya na hatimae kujaa kambani.
Simba walirejea kambani baada ya Okwi kufunga goli kwa mkwaju wa penati kutokana na Okwi kukwatuliwa katika eneo la hatari na kuufanya ubao kusomeka 2-1.
Ikiwa imesalia dakika 1 zile dakika 90 za uwanjani zitamatike Paul Nonga afuta kabisa ndoto za vinara hao kuondoka na pointi tatu katika uwanja wa CCM Kambarage na kufanya dakika 90 zimalizike kwa sale 2-2..

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.