Lwandamina: Dakika 20 Za Kwanza Tu >>>>>
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, 'George Lwandamina' amesema tayari amewapanga vijana wake kuhakikisha wanapambana dakika zote 90 ili kuhakikisha wanaondoka na ushindi uganini katika mchezo wa leo. Yanga ambao leo wanashuka dimbani kumenyana na St Louis katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika.
Aidha Lwandamina amewatahadharisha wachezaji wake kuwa makini kwa dakika 20 za kipindi cha Kwanza na kuhakikisha wanatangulia kufunga.
“ tumejipanga vyema kushinda mchezo wa leo. Nimewapanga vijana kuwa makini dakika zote 90 lakini nimewaambia kuwa makini zaidi na dakika 20 za kwanza . Tunahitaji kutangulia kufunga na kumiliki mpira”
George Lwandamina
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa awali uliopiga uwanja wa taifa Yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa goli 1
-0 goli lililopachikwa kimiani na Juma Mahadhi.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.