Sababu zinazowafanya wanaume kutamani wanawake wengine hata ikiwa wameoa



Ni nadra kukutana na mwanaume asiyepindua shingo pindi anappokutana na kipusa mrembo hata ikawa ameoa

Kwa mujibu wa mtandao mmoja uliofanya utafiti juu ya suala hili uliweza kuwauliza wanaume kupitia kwenye ukurasa wa Facebook sababu zinazowafanya watamani wanawake wengine licha ya wao kuwa kwenye ndoa na wakatoa majibu ya kusisimua.


1. Wanaume huwatizama wanawake kwa tamaa kwa sababu walivyoumbwa kwa nakshi
2. Kwa sababu utatamani gari la Mercedez licha ya kuwa mmiliki wa gari la aina ya Toyota
3. Kwa sababu wanaume wote wana tabia sawa ya kuvutiwa kupitia kwa macho
4. Wanafanya hivyo kwa sababu wanawatafuta wanawake ambao ni magwiji kitandani
5. Kwa sababu wao ni binadamu tu lazima watamani
6. Kwa sababu mfalme Suleimani katika Biblia hakuwa na mke mmoja
7. Wanafanya hivyo kubaini iwapo wanawake wote wako na maumbile au sifa zinazofanana
8. Ni njia ambayo Mungu aliwaumba, hata mfalme Daudi wa agano la kale katika Biblia pia alikuwa akiwatizama wanawake akiwamezea mate
9. Huwa hawaridhiki kwa kile wanachopatiwa na wake zao, lazima watafuta kuridhishwa kwingine
10. Huezi ukala ugali kila siku ilhali unaeza badilisha lishe kwa kula Pizza
11. Macho hayana pazia
12. Kitu kizuri huvutia na bila shaka lazima mtu akitamani

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.