HONGERA AZAM FC


Mwaka 2008, klabu ya Azam ilianzisha kituo cha kulea na kuendeleza vipaji, yaani akademi.

Kituo hicho kilianza kwa asilimia kubwa na vijana waliokuwemo kwenye kikosi cha Copa Coca Cola cha Tanzania kilichoshinda ubingwa wa dunia huko Brazil.

Jukumu Kibanda, Joseph Mahundi, Faraji Hussein, Karim Sule,  Kabali Faraji na Himid Mao ni miongoni mwa wachezaji hao.

Akademi hiyo ikazidi kukua mwaka hadi mwaka ambapo baadaye vijana wengine kama Tumba Lui, Rashid Mandawa 'Chidi Kidebe', Mohamed Hussein 'Tshabalala', Saimon Msuva na Cosmas Lewis 'Balotelli' wakajiunga na kituo hicho.

Leo, miaka kumi baadaye, akademi ya Azam FC imetoa wachezaji wengi wanaotamba kwenye vilabu mbalimbali Tanzania na nje ya nchi.

Timu ya taifa ya Tanzania, inaundwa na asilimia zaidi ya 50 ya mazao ya Azam FC.

Katika orodha ya wanaosakata soka nje, unaweza ukawaondoa Rashid Mandawa na Saimon Msuva kwa sababu tiketi zao za huko zikitokea sehemu nyingine...japo ukiwaweka katika orodha hiyo, hupati dhambi.

Lakini Himid Mao, Shaaban Idd Chilunda, na Farid Mussa Malick ni matunda ya moja kwa moja ya Azam FC kucheza nje ya Tanzania.

Na sasa ni Yahya Zayd, zao jingine la akademi ya Azam FC linalokwenda kupeperusha bendera ya Tanzania nje ya Tanzania.

Hii ndiyo maana ya Timu Bora, Bidhaa Bora.

Viva Azam FC!

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.