Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 30.08.2018 Neves, Toure, Choupo-Moting, Rose, Chadli, Pogba



Manchester City ina wasiwasi Manchester United itawapiku katika hatua yao kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Ureno Ruben Neves mwenye umri wa miaka 21 kutoka Wolves. (Goal)

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure, mwenye miaka 35, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kurudi Olympiakos. (Mirror)

Paris St-Germain wako tayari kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Stoke na Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting, mwenye umri wa miaka 29. (Sun)

Beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose, bado anatarajia kuendelea kuwa katika klabu hiyo baada ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Ijumaa. (Mail)

Danny Rose, bado anatarajia kuendelea kusalia Tottenham

Winga wa Ubelgiji Nacer Chadli, mwenye umri wa miaka 29, anataka kuihama West Brom kabla ya Ijumaa. (Telegraph)

Barcelona ina imani ya kumsajili wachezaji wawili wa kiungo cha kati waliowalenga msimu ujao wa joto. Wachezaji hao ni Paul Pogba, wa manchester united na wa Paris St-Germain' raia wa Ufaransa Adrien Rabiot, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Ajax Frenkie De Jong. (Sport)

Mchezaji anayelengwa na Barcelona De Jong anasema atasalia Ajax, lakini mchezaji huyo wa kiungo cha kati raia wa Uholanzi bado hajakataa uhamisho kwenda Nou Camp katika siku zijazo. (NOS)
De Jong anasema atasalia Ajax

Kipa wa Atletico Madrid raia wa Slovenian Jan Oblak, mwenye umri wa miaka 25, hana nia ya kurefusha upya mkataba wake na klabu hiyo ya La Liga club. (AS)

Winga wa England Jason Puncheon, mwenye umri wa miaka 32, anapigwa jicho na Middlesbrough wakati Tony Pulis akitazamia kuungana upya na mchezaji huyo wa Crystal Palace. (Teesside Gazette)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Everton raia wa Uhispania Sandro Ramirez, mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kujiunga na Real Sociedad kwa mkopo kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ijumaa. (ESPN)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Arsenal Reiss Nelson, aliye na miaka 18, anbatarajiwa kujiunga na timu ya Ujerumani Hoffenheim kwa mkopo. (ESPN)

UD Ibiza inataka kumsajili Antonio Cassano

Klabu ya Uhispania daraja la tatu UD Ibiza inataka kumsajili mchezaji wa timu ya taifa ya Italia kiungo cha mbele Antonio Cassano, aliye na miaka 36. (Corriere della Sera)

Sevilla inakaribia kumsajili winga wa Uholanzi Quincy Promes, mwenye miaka 26, kutoka Spartak Moscow katika mkataba wa thamani ya Euro milioni 20. (AS)


Mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 23, anatarajiwa kuondoka Liverpool kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho Ulaya huku Besiktas ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomuwania mchezaji huyo. (Liverpool Echo)

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.