Taifa Stars yajifua Boko, Manula nje


Wachezaji wa Timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, wameanza mazoezi leo asububi katika uwanja wa Boko Veteran, Dar es Salaam.


Wachezaji waliongezwa jana Salum Kihimbwa, Salum Kimenya, Kelvin Sabato, Paul Ngalema, Ally Abdukadir, Frank Domayo na David Mwantika wote walikuwepo uwanjani hapa.


Katika mazoezi hayo kocha Emmanuel Amunike alianza kwa mbinu za kuhakikisha wachezaji hao wanatulia na mpira chini katika kupeleka mashambulizi.


Pia akihakikisha anatumia winga za pembeni katika kupitisha mashambulizi yake na kumtumia Salum Kihimbwa.


Uwezo wa kihimbwa katika kutulia na mpira na spidi yake vilionekana kumvutia kocha Amunike, kwani kila alipokuwa akishika mpira mchezaji huyo alikuwa akionyesha kuvutiwa naye.


Wakati mazoezi hayo yakiendelea kipa Aish Manula ambaye ni mchezaji pekee wa Simba, alikuwepo uwanjani hapa lakini alikuwa hafanyi mazoezi na wenzake yeye alikuwa akifuata kila maelekezo yaliyokuwa yakitolewa.


Wachezaji wote waliohudhuria mazoezi hayo ni Aish Manula, Aggrey Morris, Kelvin Sabato, Salum Kihimbwa, Salum Kimenya, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Yahya Zaiid, Abdukadir Ally,Paul Ngalema, David Mwantika na Mohammed Abdulrahman.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.