Simba Waitaja Timu Watakayocheza Nayo Siku Ya Simba Day


Uongozi wa Simba umethibitisha leo Jumatano kuwa itacheza na timu Asante Kotoko ya Ghana katika maadhimisho ya Simba Day Agosti 8.
Uongozi huo umetoa taarifa hiyo leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Serena Hoteli jijini hapa, huku wakieleza kwamba baada ya timu hiyo kucheza mchezo wake wa kirafiki wachezaji watafanyiwa tafrija fupi katika hoteli ya Serena.
Simba ambayo imeweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki, itakutana na Kotoko ambayo imechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Ghana mara 21 na taji la Klabu Bingwa Afrika mara mbili.
Kocha Patrick Aussems leo atakuwa kwenye benchi la ufundi kwa mara ya kwanza akiingoza Simba katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mouloudia Oujda ya Morocco.
“Taarifa ambazo zilikuwa zikienea kwamba tutacheza dhidi ya AFC Leopard kutoka Kenya si za kweli na tutacheza na hiyo ambayo tumeitaja.
"Mbali ya mechi hiyo tunatangaza rasmi wiki ya Simba ambayo imeanza leo na tutakuwa na mambo mengi ambayo tutayafanya katika maji, " alisema Haji Manara Ofisa Habari wa Simba.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.