Mbeligiji Simba ataja sababu za kuwapiga benchi baadhi ya wachezaji akiwemo 'Mo' Ibrahim
Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, amefunguka na kuweka hadharani sababu za kiungo wake, Mohammed Ibrahim kutokupata nafasi.
Tangu msimu wa ligi uanze, kiungo huyo hajapata nafasi ya kucheza kutokana na upana wa kikosi hicho ambao una wachezaji wa kila aina kulingana na usajili ambao imeufanya.
Mbeligiji amesema kikosi cha Simba ni kipana na kina wachezaji walio na ushindani, hivyo hawezi akamuanzisha kama waliopo kwenye kile cha kwanza wanafanya vizuri.
Aussems ameeleza kujituma kwa mchezaji ndiyo kutamfanya apate namba kwenye kikosi chake hivyo kama Ibrahim anataka namba inabidi apambane.
Kocha huyo tangu atue nchini kuanza kibarua na wekundu hao wa Msimbazi, hajapoteza mchezo hata mmoja uwe wa kirafiki au wa kimashindano mpaka sasa.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.