Jadidi ya Msuva out CAF Champions league.
Klabu ya Difaa El Jadidi ya nchini Morocco anayochezea winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva imeng’olewa rasmi katika michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na TP Mazembe ya DRC.
Katika mchezo huo ambao umepigwa usiku wa jana mjini Lubumbashi nchini Congo, ulishuhudiwa kiungo huyo wa Tanzania akicheza dakika zote tisini na kuisaidia timu yake kusawazisha bao dakika ya tisini, dakika tatu baada ya kuwa nyuma kwa bao moja la TP Mazembe lililofungwa dakika ya 87.
TP Mazembe inasonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kuongoza kundi B kwa alama 12 ikifuatiwa ES Setif ya Algeria ambayo imemaliza hatua hiyo kwa alama nane.
Difaa El Jadidi imemaliza hatua ya makundi ikikamata nafasi ya tatu kwa alama sita ambazo zinawaondoa katika michuano hiyo pamoja na klabu ya MC Alger ya Algeria iliyomaliza mkia kwa alama tano pekee.
Klabu zilizofuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ni Al Ahly ya Misri, TP Mazembe ya Congo DRC, Wydad AC ya Morocco, 1 de Agosto ya Angola, Horoya AC ya nchini Guinea na Esperance pamoja na Etoile du Sahel za Tunisia.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.