Maneno ya kocha wa Rayon Sports kuelekea Mchezo dhidi ya Yanga sc leo
Kocha mkuu wa klabu ya Rayon Sports, Roberto Oliviera Goncalves De Calmo amesema kuwa wanatazamia kuwa na mchezo mgumu dhidi ya Yanga sc leo.
Rayon inatarajiwa kushuka dimbani leo jumatano kuwaarika wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Africa, Yanga katika pambano linalotarajiwa kuanza majira ya saa 10 jioni ya leo katika uwanja wa Nyamirambo.
Akizungumza muda mchache kabla ya Mchezo kocha huyo amesema: "Tunatarajia mchezo mgumu , Tumekuwa na muda wa kutosha kujiandaa kwa mchezo huu muhimu".
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.