Manara aitumia Manchester City kuitetea Simba sc.
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameendelea kutoa ufafanuzi kwa mashabiki wa klabu hiyo huku akiwatolea mifano kwa vilabu vikubwa ulimwenguni.
Hii ni kutokana na kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kikihusisha mashabiki wa klabu hiyo ya Wekundu wa msimbazi kuwatupia lawama viongozi juu ya kiwa cha timu yao ukilinganisha na thamani ya wachezaji na gharama za maandalizi.
Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ambao ndio amekuwa akiutumia kwa sehemu kubwa kuwasiliana na mashabiki wa klabu hiyo ameandika ujumbe alioambatanisha na picha ya matokeo ya klabu ya Manchester City ya nchini England ambayo kwa siku ya jana ilitoa sare ya goli 1-1 na klabu ya Wolverhampton
Tofauti ya thamani ya Man City na Wolverhampton ni Mbingu na Ardhi kwa hadhi yoyote ile..iwe kwa thamani ya wachezaji na hata umaarufu wa team zenyew.lakini jioni hii zimetoka sare 1-1.. hii maana yake nn? Matokeo ya mpira sometimes hayategemei ukubwa wa club au wapi ulipojiandaa..hilo linaangaliwa mwisho wa ligi nani yupo wapi!! Pata picha fans wa mapacha wa kkoo team zao zitoke sare na Biashara Mara au Ndanda!! 🤔🤔