Makubwa ya James Kotei Simba.
Beki wa kati wa klabu ya Simba, Mghana James Kotei amesema malengo yake katika klabu yake kwa msimu huu ni kuhakikisha timu hiyo inatetea vyema ubingwa na ligi kuu Tanzania bara na kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema katika michuano ya CAF Champions league.
Akizungumza na mtandao wa soka255east.com Kotei amesema " Malengo yangu katika msimu huu ni kuisaidia timu yangu kutetea ubingwa wa ligi na kuhakikisha inafanya vyema katika michuano ya CAF Champions league"
James Kotei ni miongoni mwa wachezaji nane wanaitumikia ligi kuu Tanzania bara wakitokea Ghana ambao ni – Nicholas Gyan, Kwasi Asante, Yakubu Mohammed, Enock Atta Agyei, Razak Abalora, Daniel Amoah and Hans Kwofie
Kotei alijiunga na Simba mnamo mwaka 2016 kwa mkataba wa miezi 6 na kuongezewa mkataba wa miaka miwili baada ya kufanya vizuri katika kipindi hicho.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.