DABI ya Mashemeji, mashabiki wang'oa viti uwanjani.
Kichapo cha mabao mawili kwa sifuri walichokipata AFC Leopards ya Kenya katika DABI ya Mashemeji jana kwenye Ligi Kuu nchini humo, kimewafanya wavunje viti jukwaani.
Leopards ambao walimabulia kichapo cha mabao 2-0 waliamua kuvunja viti kufuatia Gor Mahia kufunga bao la pili kupitia kwa Benard Ondiek mnamo dakika ya 38 kipindi cha kwanza na kudai kuwa aliotea.
Kitendo cha hasira hizo za mashabiki kiliwafanya mashabiki wa timu hiyo kuja juu na kuamua kuvunja viti huku wakimtupia lawama Mwamuzi wa mchezo baada ya bao la Ondiek kuzama kimiani.
Maamuzi ya mashabiki hao yanakumbusha kitendo ambacho walikifanya mashabiki wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam misimu takribani miwili iliyopita kwa kuvunja viti baada ya Tambwe kufunga bao huku akiugusa mpira na mkono.
Baada ya ushindi huo, Gor Mahia ainayoongozwa na Kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi nchini humo na ikifikisha wa taji la 17.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.