Wawili Simba Kwenda Kenya Kuongeza Nguvu Kikosini Kuhakikisha Inatwaa Ubingwa Wa SportPesa Super Cup.


Klabu ya Simba Sc baada ya kufanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Sportpesa Super cup imepanga kuongeza wachezaji wawili kwenye kikosi kitakachocheza Fainali na Gor Mahia siku ya Jumapili june 10.

-Simba wameamua kufanya hivyo baada ya kuona wapinzani wao Gor Mahia ya Kenya wana kikosi kizuri kuliko wao pia sheria za mashindano hayo zinawaruhusu klabu ya Simba kuongeza wachezaji wawili mwanzoni walikuwa wachezaji 17 ikamuongeza Adam Salamba wakawa 18 na Sheria ya mashindano hayo ni kutumia wachezaji 20 hivyo Simba wana nafasi ya kuongeza wachezaji 2.

-Kocha Masoud Djuma ameuomba uongozi wa klabu hiyo kufanya mpanga wa kuwawasilisha Kenya beki Asante Kwasi na Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi ili waweze kuongeza msaada kwa kikosi hicho.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.