Simba Yawa Ya Kwanza Kunusa Ubingwa SportPesa Super Cup.
Timu ya Simba imekuwa ya kwanza kutinga hairs ya fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega Homeboyz kwa mikwaju ya penati 5-4.
Simba imeingia hatua hiyo ikiwa safu yake ya ushambuliaji haijafunga bao hata moja katika muda wa kawaida kitu ambacho wanapaswa kukifanyia kazi katika mchezo wa fainali.
Leo Simba ilicheza vizuri kwa kasi kuliko katika mchezo uliotangulia huku wakimiliki sehemu kubwa ya mechi hiyo.
Mchezo uliopita dhidi ya Kariobangi Sharks, Simba iliibuka na ushindi wa penati 3-2.
Penati za Simba zilifungwa na Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Shiza Kichuya na Jonas Mkude wakiwa hawajakosa hata moja.
Simba inasubiri mshindi kati ya timu za Gor Mahia dhidi ya Singida United ambapo mchezo wao unaanza muda si mrefu.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.