Kocha Simba Akana Kujiuzulu, Adai Hayo Ni Maneno Ya Mitandaoni.

Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kuwa hana nia ya kujiuzulu wala hajajiuzulu kama ilivyoenezwa kwenye mitandao ya kuwa yeye amejiuzulu.

Djuma ameyasema hayo mara baada ya kuanza kuenea taarifa za yeye kubwaga manyanga kuinoa Simba huku akiweka msisitizo wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mkataba wake utakapo malizika.

Acheni kusikiliza maneno ya Mtandaoni ya kusema kama mimi nimejiuzulu, hayo maneno sijui yalipotoka, muulizeni huyo aliyoyaleta muulizeni alikoyatoa. Ninamkataba na Simba mpaka mwakani na inshallah kwa Nguvu za Mungu nikamilishe mkataba wangu.

Djuma alijiunga na Simba akichukua mikoba ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo mgaMga Jackson Mayanja alieachia ngazi mnamo October 18 2017 na kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.