Azam Yaipiku Yanga Yamnasa Nyota Huyu Na Kumpa Mkataba Wa Miaka Miwili.


Mshambuliaji wa Njombe Mji Ditram Nchimbi amesajiliwa na klabu ya Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Licha ya timu yake kushuka daraja, Nchimbi ni mmoja wa washambuliaji waliofanya vizuri msimu uliopita.

Nchimbi alikuwa akipigiwa 'chapuo' na wadau kwa uongozi wa Yanga ili asajiliwe hasa baada ya mwenyewe kuweka wazi kuwa yuko tayari kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.

Nchimbi amekuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Azam FC baada ya Kutinyu na Ngoma.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.