Yanga Watolea Ufafanuzi Swala La Yondani Kutokomea Kusikojulikana.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema sio kweli kuwa beki kisiki wa timu hiyo Kelvin Yondani ametoweka klabuni na hajulikani aliko.
Mkwasa amesema mchezaji huyo aliwapa taarifa kuwa ana matatizo ya kifamilia na wanatarajia ataungana na kikosi cha Yanga ambacho wakati wowote kinachotarajiwa kwenda nchini Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.
Kumekuwa na presha kubwa kwa Yanga wakati huu wa usajili baada ya kuelezwa baadhi ya wachezaji wake ambao wamemaliza mikataba wanawindwa na timu nyingine.
Yondani ni miongoni mwa wachezaji waliomaliza mikataba lakini imeelezwa kuwa tayari uongozi wa Yanga umeshakaa nae mezani.
Yondani anawindwa na klabu za Simba na Azam FC wakati Juma Abdul nae anahusishwa kutua Azam FC.
Obrey Chirwa mkataba wake unamalizika Juni 30, 2018. Nae ni miongoni mwa wachezaji wanaodaiwa kuwindwa na vilabu vya Simba na Azam FC.
Yanga ina wachezaji 10 waliomaliza/wanaomaliza mikataba yao ambao ni Benno Kakolanya, Hassani Kessy, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Andrew Vicent, Nadir Haroub, Said Juma Makapu, Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya na Emanuel Martin
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.