Hii Hapa Taarifa Mpya Kutoka Simba sc Muda Huu



Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka kesho Alhamisi, May 31 kwenda nchini Kenya kushiriki michuano ya Sportpesa Super Cup.

Mabingwa hao wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu wataondoka saa moja asubuhi na ndege za shirika la KQ.

Simba itacheza mchezo wake wa kwanza Juni 04 dhidi ya K. Sharks. Mchezo utapigwa kwenye dimba la Kasarani jijini Nairobi ukitarajiwa kuanza saa tisa alasiri.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.