Yanga Kurejea Leo Mchana



Kikosi cha timu ya Yanga kitarejea nchini mchana wa leo kutoka Algeria ilipokuwa na mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Yanga imeanza vibaya hatua hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa wenyeji USM.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema kikosi kitarejea na moja kwa moja itaanza maandalizi ya mechi za ligi.

Mkwasa amesema licha ya kukubali kipigo hicho kikubwa lakini vijana wake walijitahidi kupambana ila makosa madogo madogo ndio yaliwagharimu.

"Kikosi kitawasili nchini mchana wa leo wachezaji watapumzika na baadae tutaanza maandalizi ya mechi zetu za ligi," alisema Mkwasa.

Mei 10 Yanga itasafiri kwenda jijini Mbeya kucheza na Tanzania Prisons.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.