WASHIRIKI WA YANGA WAPATA DILI, KUCHEZA NA HULL CITY KUTOKA UINGEREZA


Na Joseph michael
-Mabingwa wa ligi ya kandanda nchini Kenya Gor Mahia watakabiliana na klabu ya Uingereza Hull City jijini Nairobi.

-Hull City, ambayo hushiriki katika ligi ya daraja la pili EFL nchini Uingereza wanatarajiwa kuwasili siku ya Ijumaa kwa mechi ya kirafiki siku ya Jumapili katika uwanja wa Kasarani..

-Ziara ya klabu hiyo barani Afrika inafadhiliwa na kampuni ya Kamare ya Sportpesa kutoka kenya ambayo ni mfadhili wa timu tatu.
Tayari Hull City imetuma ujumbe unaoongozwa na mchezaji wa zamani Dean Windass.

-''Ijapokuwa baadhi ya wachezaji huenda wamechoa kutokana na msimu huu nina hakika kwamba wataonyesha mchezo mzuri'', alisema Windas alipopwasili Kenya.
-Ziara hiyo ya Hull City inajiri mwaka mmoja baada ya Gor Mahia kucheza na kupoteza 2-1 dhidi ya timu ya ligi ya Premier nchini Uingereza Everton katika mechi nyengine ya kirafiki iliochezwa katika uwanja wa kitaifa wa Dar es Salaam.

-Mwaka uliopita Hull City iliochezesha vijana wadogo iliishinda timu Kenya All Star 2-1 nchini Uingereza.

-Hull City ilishushwa daraja kutoka katika ligi ya UIngereza mwisho wa msimu 2016/2017na sasa wako katika nafasi ya 18 katika orodha ya timu 24 za daraja la pili huku ikiwa imesalia mechi mbili pekee msimu kukamilika.

-Gor Mahia ilijikatia tiketi ya kucheza dhidi ya klabu ya pili ya Uingereza chini ya mwaka mmoja baada ya kuishinda klabu ya AFC Leopard 5-4 kwa njia ya penalti katika uwanja wa Afraha
 - Kuwa nasi muda wote sisi tunajua kile unachokipenda!

Joseph michael

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.