Post Ya Haji Manara Mara Baada Ya Simba Kutwaa Ubingwa VPL

Baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom msimu huu, Afisa habari wa Simba Haji Manara amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyoifanya kuhakikisha Simba inatwaa ubingwa baada ya kusubiri kwa misimu mitano.

Manara pia amewapa pongezi maalumu mashabiki wa Simba kwa kuwa pamoja na timu wakati wote na kila mahali.

"Hongereni washabiki wetu...ubingwa huu ni wenu..mmetushangilia popote tulipokuwa..mmetuombea siku zote...jivunieni ubingwa huu..nyie na wachezaji ndio mnaostahili kupongezwa kipekee...Thanks our fans🙏🙏🇮🇩🇲🇨🇲🇨," amesema Manara

Simba imetwaa ubingwa baada ya Yanga kufungwa mabao 2-0 na Tanzania Prisons kwenye mhezo wa ligi kuu ya vodacom uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine leo.

WACHEZAJI SIMBA WAKISHANGILIA UBINGWA VPL

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.