Pambazuka Na Tetesi Za Usajili Ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara Vodacom Premier league 25/05/2018
Stand United wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa jku feisal Salum na wana matumaini ya kukumilisha taratibu hizo mda wowote kuanzia sasa
Azam fc wameanza mazungumzo na Lipuli fc ya kumsaini mshambuliaji Adam salamba , lakini Lipuli fc wanataka milioni 40 - 50
Mchezaji anayewindwa na Mwadui fc ya mkoani Shinyanga Beno Kakolanya atafanya mazungumzo na timu ya Jkt Tanzania wiki hii huku beno mkataba wake unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu
Yanga sc watahitaji kulipa milioni 30 kumsaini mlinzi Seleman kihimbwa wa Mtibwa Sugar
Beki kisiki wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania shadrack sajingwa sasa ni kocha wa msaidizi wa klabu ya Yanga sc anaweza kurudi kuwa kocha mkuu wa timu ya vijana ya yanga B
Pia imeripotiwa kuwa Singida wamejiunga kwenye mbio za kumsaini Golikipa wa Mtibwa Sugar Benedicto tinocco
Mbeya City na Kagera Sugar wote wanataka kumsaini mshambuliaji wa Kelvin sabato anapatikana kwa milioni 15
Klabu ya yanga sc inatamani kumwinda mchezaji wa Simba sc zimbwe Jr
Imeripotiwa kuwa Golikipa wa klabu ya Yanga sc Rostand ameoneshewa mlango wa kutokea hii ni kutokana na kushuka kwa kiwango
Klabu ya Alliance School ya Jijini Mwanza ipo mbioni kuinasa saini ya kocha kutoka Rwanda baptisha kayirange
@bwajideo.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.