MROMANIA WA AZAM FC OUT, HANS VAN PLUJIM IN
Na Joseph michae
-Kocha Mkuu wa klabu ya Azam, Aristica Cioba amuamua kuwaaga mapema waajiri wake klabu ya Azam Fc na kuondoka nchini kurejea kwao Romania.
-Kocha huyo ameamua kuchana na klabu ya Azam FC huku akiwa amebakisha miezi miwili katika mkataba wake ambao unaisha mwezi Julai mwaka huu.
-Klabu ya Azam ilikuwa na mpango wa kuachana moja moja na kocha huyo mwisho wa msimu huu ila kocha huyo amesimamishwa na kamati ya masaa 72 kwa kumtolea maneno machafu mwamuzi wa mchezo dhidi ya Njombe Mji.
-Kwa sasa Suala lake limepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ili kutolewa adhabu baadae Cioaba alitonywa anaweza kufungiwa mechi 3 na faini huku klabu ya Azam Fc imebakiza mechi 4 kumaliza msimu huu.
-Aristica Cioaba alijiunga na Azam mwezi january mwaka jana alisaini mkataba wa miezi sita na aliongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao utaisha July mwaka huu.
-Klabu ya Azam na Cioba wamechana rasmi na sasa klabu hiyo imemalizana na kocha wa kikosi cha Singida United, Hans Van Plujim. ambaye atakuwa kocha mpya wa klabu hiyo msimu ujao.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.