Manara Kutema Nyongo Jumanne Hii.


Wekundu wa Msimbazi Simba tayari wameshatangazwa kuwa mabingwa rasmi wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 baada ya Yanga kufungwa na Tanzania Prisons, hivyo Simba leo kacheza game yake dhidi ya Singida kama sehemu ya kukamilisha ratiba.

Simba akiwa ugenini amecheza game dhidi ya Singida United na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, goli la Simba likifungwa na Shomari Kapombe dakika ya 23 ya mchezo, hivyo sasa Simba wanapambani kumaliza Ligi na kuweka rekodi ya kutwaa Ubingwa bila kupoteza mchezo.

Baada ya ushindi dhidi ya Singida afisa habari wa Simba Haji Manara aliahidi kuwa wakichukua Ubingwa atasema sana vipi? “Niwaombe kwenye press conference yangu ya kwanza Jumanne Dar es Salaam yale madukuduku yangu mtayasikia nitasema hadi mashabiki wa Yanga wajitoe katika mitandao ya kijamii”>>> Haji Manara

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.