MADRID YATANGULIA FAINALI ULAYA


Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Ulaya wameingia fainali ya michuano hiyo Licha ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 mtange uliofanyika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mchezo huo nusu fainali ya pili Bayern walitawala  sehemu kubwa ya mechi hiyo lakini idara yao ya ushambuliaji ilikuwa butu.

Bayern walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tatu ya mchezo lililofungwa na Joshua Kimmich.

Karim Benzema aliisawazishia Real bad hilo dakika ya 11 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 46.

Kiungo James Rodriguez aliisawazishia Bayern bao hilo dakika ya 63 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya mlinda mlango Kaylor Navas kuokoa shuti lake.

Madrid atacheza na mshindi kati ya Liverpool au AS Roma ambao wanakutana kesho kwenye nusu fainali ya pili ya michuano hiyo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.