Lipuli Wasema Wamepokea Barua 2 Za Salamba Moja Ni Ile Ya Yanga Sc.


Klabu ya lipuli imethibitisha kuwa  klabu za Yanga na Azam fc zimeleta barua za kumtaka mshambuliaji wa klabu hiyo Adam Salamba.

Taarifa hiyo imejiri baada ya hapo jana klabu ya Yanga kutoa taarifa ya kuiandikia klabu ya Lipuli barua ya Kumtaka Salamba kwa kipindi hiki ambacho Yanga inashiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Lipuli zinaeleza kuwa ni kweli barua hiyo imewasili klabuni hapo na moja ya yaliyoaandikwa kwenye barua hiyo ni pamoja na kumuhitaji mchezaji huyo kwa michezo ya makundi ya CAF Confederation Cup lakini pia kumhamisha moja kwa moja.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kwa kusema kuwa licha ya Yanga klabu nyingine ambayo imewasilisha barua ya kumuhitaji Salamba ni klavu ya Azam fc.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.