KOCHA NGORONGORO HEROES AMMY NINJE AAHIDI USHINDI DHIDI YA MALI JUMAPILI

 
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes) Ammy Ninje ameahidi ushindi katika mchezo wao wa raundi ya pili kufuzu fainali za Africa za Vijana dhidi ya Mali utakaochezwa Jumapili Mei 13,2018 kwenye Uwanja wa Taifa.

Ninje amesema Mali ni timu nzuri ambayo amekuwa akiifuatilia kwa karibu lakini kwa upande wao wamekuwa katika maandalizi ya kuhakikisha wanafanya vizuri na wachezaji wanaonekana kuyashika vyema mafunzo yake.

Amesema hata kambi ya kikosi hicho imekuwa na morali kubwa yenye kiu ya kutaka kufanya vizuri na kufuzu kwenda raundi ya Tatu ambayo ndio ya mwisho kabla ya kufuzu kucheza fainali hizo za Africa kwa vijana.

Amewataka waTanzania kujitokeza kwa wingi Jumapili ili kuwaongezea nguvu zaidi  vijana hao ya kufanya kile ambacho wa Tanzania wengi wangependa kukiona.

Naye Issa Makamba nahodha wa kikosi hicho amesema wachezaji wako tayari kwa mapambano ambayo wanaamini watashinda.

Katika mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni Kiingilio kwa VIP zote shilingi 3,000 na Mzunguko shilingi 1,000.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.