Jerry Muro Atupa Kombora Kwa Manara Baada Ya Kuwarushia Kombora Yanga, Je Unaikumbuka Ishu Ya Simba Kushindia Mihogo?.



Inapofika ishu ya utani wa jadi asikwambie mtu hapa kila mmoja hutoa lililoko moyoni..
Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara na aliyekuwa Afisa habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro wamerushiana maneno kunako mtandao wa Instagram mara baada ya Manara kuposti ya video ya goli la Bale huku akiandika caption yenye kusomeka hivi.
Goli la Bale. ..linaweza kukufanya usahau kuwa Wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara miezi 3 mfulululizo

Katika majibizano hayo Muro alianza kwa kumrushia kijembe  Manara kwa fumbo na Manara Kurejesha huku akimkumbusha kuhusiana na ishu ya kushindia Mihogo.

Majibizano hayo yalikuwa  kama ifuatavyo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.